1. MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA ELIMU.
1.1. Dhana ya Elimu katika Uislamu.
§
Katika Uislamu Elimu maana yake ni:
-
Ujuzi unaoambatana na utendaji au
-
Mabadiliko ya tabia yanayoambatana (yanayotokana) na
ujuzi au
-
Ujuzi unaomuwezesha mtu kufanya (kutenda) jambo kwa
ufanisi au inavyotakikana.
§
Nani
aliyeelimika? (Sifa za mtu aliyeelimika).
-
Aliyeelimika ni yule mwenye ujuzi unaomuwezesha kutenda
(kufanya) jambo kwa ufanisi na inavyotakikana.
-
Mjuzi wa Qur’an na Sunnah ni yule anayeendesha kila
kipengele cha maisha yake ya binafsi na kijamii kwa mujibu wa Qur’an na Sunnah.
-
Watakapo fanana kimwenendo na kitabia wale wenye elimu
na wasiokuwa na elimu, basi wenye elimu watakuwa hawajaelimika ila wamesoma tu.
“……………Sema, Je! Wanaweza kuwa sawa
wale wanaojua na wale wasiojua? Wanaotanabahi ni wale wenye akili tu………”(39:9).
§
Nafasi ya Elimu katika Uislamu.
-
Nafasi ya elimu na mwenye elimu katika Uislamu
inaonekana katika maeneo yafuatayo;
i.
Elimu ndio takrima ya kwanza
aliyopewa mwanaadamu na Mola wake kama nyenzo
pekee itakayomuwezesha kumjua Mola wake na kumuabudu vilivyo.
“Na (Mwenyezi Mungu) akamfundisha
Adam majina ya (fani za) vitu vyote” (2:31) na pia rejea (2:38).
ii.
Elimu ni amri ya kwanza kwa mwanaadamu
kuitafuta kama alivyoamrishwa kusoma Mtume
(s.a.w).
“Soma kwa jina la Mola wako
aliyeumba……..” (96:1-5).
§
Kwa nini
Elimu imepewa nafasi ya kwanza katika Uislamu?
1.
Ndio nyenzo pekee inayomuwezesha mwanaadamu kumtambua
Mola wake na kuweza kumuabudu ipasavyo.
“Kwa hakika wanaomuogopa
(wanaomuabudu) Mwenyezi Mungu ipasavyo miongoni mwa waja wake ni wale
wataalamu” (35:28).
2.
Elimu iliyosomwa kwa murengo wa Qur’an na Sunnah ndio
inayomuwezesha muumini kuwa Khalifa (kiongozi) wa Allah (s.w) hapa ulimwenguni.
“Na kumbukeni aliposema Allah
kuwaambia Malaika kwamba ataweka ardhini khalifa (kiongozi)” (2:30) pia rejea
(2:38).
3.
Kutafuta elimu ni ibada maalum yenye hadhi kubwa kuliko
ibada zote mbele ya Mwenyezi Mungu (s.w) inayopelekea mja kufanya ibada
vilivyo.
“……Na (waumini) waliopewa elimu
watapata daraja (kubwa) zaidi…” (58:11).
4.
Mwenye elimu ndio ana nafasi bora ya kumtambua na
kumuabudu Mola wake ipasavyo kwa kila kipengele cha maisha yake.
Rejea Qur’an (35:28), (39:9) na (58:11).
§
Nini
Chanzo cha Elimu?
-
Chanzo cha Elimu na fani zote ni ALLAH (S.W) ambaye
humuelimisha mwanaadamu kupitia njia mbali mbali.
o
Njia anazotumia
Mwenyezi Mungu (s.w) kuwafundisha na kuwasiliana na wanaadamu ni:
1.
Il-hamu.
- Ni
mtiririko wa habari (ujumbe) unaomjia mwanaadamu bila kufundishwa na mtu yeyote
au kuona mfano wake katika mazingira yeyote.
2.
Kuongea na Mwenyezi Mungu (s.w) nyuma ya
pazia.
- Ni njia
mwanaadamu huongeleshwa na Mwenyezi Mungu (s.w) moja kwa moja kwa sauti ya
kawaida bila kumuona.
- Nabii Musa
(a.s) ni miongoni mwa Mitume waliosemeshwa na Allah (s.w) nyuma ya pazia.
Rejea
Qur’an (28:30), (7:143) na (19:23-26).
3.
Kutumwa Malaika na kufikisha ujumbe kama alivyotumwa.
- Ni njia
anayoitumia Allah (s.w) kumuelimisha mwanaadamu kwa kupeleka ujumbe kupitia
mitume na watu wengine wema.
Rejea Qur’an (53:1-12),
(15:51-66), (19:16-19), (2:102) na (3:41).
4.
Ndoto za kweli (ndoto za mitume).
- Ni kupata
ujumbe kupitia ndoto za kweli hasa kwa mitume ambayo huwa ni maagizo ya Allah
(s.w) kwa Mitume.
- Mfano ndoto
ya Nabii Ibrahim (a.s) juu ya kumchinja mwanae Nabii Ismail (a.s).
Rejea
Qur’an (37:102), (12:4-5), (12:100) na (48:27).
5.
Njia ya Maandishi (mbao zilizoandikwa).
- Ni njia ya
mawasiliano ya Allah (s.w) na waja wake kupitia maandishi yaliyoandikwa tayari.
- Nabii Musa
aliletewa ujumbe kwa maandishi kutoka kwa Allah (s.w).
Rejea
Qur’an (7:145) na (7:154).
§
Lengo kuu
la elimu katika Uislamu ni;
-
Ni kumuwezesha mwanaadamu kumtambua Mola wake vilivyo
na kuweza kumuabudu kwa usahihi na kikamilifu kwa kila kipengele cha maisha
yake ya kila siku kibinafsi, kifamilia na kijamii.
-
Ni kuweza kuyajua na kuyafuata maamrisho yote ya Allah
(s.w) na kuepukana na makatazo yake pia.
1.2. Mgawanyo Sahihi wa Elimu kwa Mtazamo wa
Uislamu.
- Kwa
mtazamo wa Uislamu elimu imegawanyika katika nyanja kuu mbili;
a) Elimu ya Mwongozo (Faradh ‘Ain).
- Ni elimu ya
lazima ambayo kila muislamu (mtu) anapaswa kuisoma, haina uwakilishi. Mfano ibada
za swala, funga, hijja, zakat, n.k.
b) Elimu ya Mazingira (Faradh Kifaya).
- Ni elimu ya
uwakilishi ambapo wakisoma wachache katika jamii inatosheleza lakini wasipopatikana wa kuwakilisha, jamii
yote itawajibika.
Mfano fani ya Udaktari, Uinjinia, Ualimu, Urubani, n.k.
1.3. Mgawanyo wa Elimu usiokubalika katika
Uislamu (usio sahihi).
- Katika Uislamu, HAKUNA mgawanyo wa ‘Elimu Dunia’ na ‘Elimu Akhera’.
- Mgawanyo huu ni potofu wenye dhana ya kikafiri
kuwa kuna maisha ya Dini yanayoongozwa na Mwenyezi Mungu na maisha ya Dunia
yanayoongozwa na binaadamu.
·
Mgawanyo
huu sio sahihi kwa sababu zifuatazo:
i.
Nabii Adam (a.s) aliandaliwa yeye na kizazi chake kuwa
Makhalifa (viongozi) na alifundishwa majina (fani zote) ya vitu vyote.
Rejea Qur’an (2:31) na (2:38-39).
ii.
Amri ya kusoma aliyopewa Mtume (s.a.w) na umma wake
haibagui elimu ya dini na dunia.
iii.
Muasisi wa (chanzo cha) elimu na fani zote ni Mwenyezi
Mungu (s.w). Hakuna mwanaadamu aliyeasisi elimu au fani yeyote ila ni
mwendelezaji tu.
Rejea Qur’an (96:3-5).
iv.
Pia Qur’an inatufahamisha kuwa wanaomcha Allah (s.w)
ipasavyo ni waumini wataalamu waliozama katika fani mbali mbali za kumjua Allah
(s.w), sio tu fani za kidini za Fiqh, Tawhiid, n.k.
Rejea Qur’an (35:27-28).
v.
Katika Qur’an Allah (s.w) anatufahamisha kuwa waumini
wenye elimu ya fani mbali mbali ndio wenye daraja kubwa zaidi mbele yake.
Rejea Qur’an (58:11), (49:13).
vi.
Hakuna mgawanyo wa elimu unaooneshwa katika Hadith za
Mtume (s.a.w) zinazoelezea fani za elimu.
- Elimu yenye Manufaa.
- Elimu yenye manufaa ni ile yenye sifa
zifuatazo:
- Ni ile inayomuwezesha mwanaadamu kumtambua na kumuabudu Mola wake vilivyo na ajili ya kufikia lengo la kuumbwa kwake.
- Ni ile inayomuwezesha mja (muumini) kuwa Khalifa (kiongozi) wa Allah (s.w) hapa Ulimwenguni.
- Ni ile inayoiwezesha jamii kuishi kwa furaha na amani ya kweli.
- Ni ile inayotafutwa na kufundishwa kwa ajili ya kupata radhi za Allah (s.w).
- Mahusiano kati ya elimu ya mwongozo na elimu ya mazingira katika Uislamu.
- Kusimama na
kuendelea kwa Uislamu katika jamii, kunategemea sana uwepo wa elimu zote mbili katika
utekelezaji wake.
- Elimu ya
mazingira pekee inapelekea kutofanyika haki na uadilifu katika jamii na kukosekana
mwongozo sahihi wa maisha ya jamii.
- Elimu ya
mwongozo pekee pia hupelekea udhaifu katika kuyamudu mazingira kutokana na
kukosekana fani mbali mbali za kimaendeleo.
Zoezi la 1.
1.
(a) Elimu ni
nini?
(b) Mtu aliyeelimika ni mtu wa
aina gani?
(c) Unatoa maoni gani iwapo
wanaojua watakuwa sawa na wasiojua kiutendaji?
2.
(a) “….Sema, Je! Wanaweza kuwa sawa wale wanaojua
na wale wasiojua?.....(39:9). Kwa
nini wanaojua hawawi sawa na wasiojua?
(b) Kwa kutumia ushahidi wa aya, onesha kuwa elimu
ndio takrima ya kwanza aliyokirimiwa mwanaadamu na Mola wake.
3.
Kwa ushahidi wa aya za Qur’an, eleza kwa nini Uislamu
umeipa elimu nafasi ya kwanza kabla ya jambo lolote?
4.
(a) Nini chanzo
cha elimu na fani zote?
(b) “Soma kwa jina la Mola wako aliyeumba…….” (96:1).
(i) Kutokana na aya hii, fafanua nini maana ya
kusoma ‘kwa jina la Allah’
(ii) Orodhesha njia tano
anazotumia Allah (s.w) katika kuwaelimisha wanaadamu.
5.
(a) Bainisha ni
upi mgawanyo sahihi na usio sahihi juu ya elimu katika Uislamu.
(b) Tofautisha kati ya elimu ya mwongozo(faradh ‘Ain)
na elimu ya mazingira (faradh kifaya).
6.
‘Mgawanyo wa Elimu Dunia
na Akhera (dini) haukubaliki (haupo)
katika Uislamu’. Eleza ni kwa nini kwa kutoa sababu zisizopungua tano.
7.
(a) Ni ipi elimu yenye manufaa?
(b) Eleza kwa
ufupi, kwa nini ili Uislamu usimame katika jamii, hatuna budi kutotenganisha ‘Elimu ya Mwongozo na Elimu ya Mazingira’?
BY MEEK HMK CLICKER
This is the only page where I got the best and exactly answers to my questions. Thanks for the help. !
ReplyDelete