Thursday, September 19, 2019

KANUNI ZA KUSOMA NA KUFAULU


KANUNI ZA KUSOMA NA KUFAULU
Kila mwanafunzi anahitaji kufaulu katika mitihani yake. Walimu nao hujisikia vizuri wakati wanafunzi wao wanapofanya vizuri katika mitihani yao.
Sasa mtu anaweza kujiuliza, kwa nini wanafunzi wengine washindwe na wengine wafaulu vizuri katika masomo na mitihani yao? Mafanikio katika masomo na kufaulu mitihani kunahitaji uwezo wa asili, kufanya kazi kwa bidii na kufuata kanunina mbmu za kusoma.
Wanafunzi wengine huona ugumu katika masomo na kufaulu mitihani, si kwa sababu hawana akili, bali hawafuati mbinu na kanuni fulani za kusoma na kufaulu mitihani. Wengi wana uwezo mzuri, kama watajifunza mbinu hizi. Mbinu na kanuni hizi zinaweza kutumiwa na wanafunzi wa shule za msingi, markaz za dini, sekondari vyuo na hata vyuo vikuu.

Kanuni za Kusoma ni kama ifuatavyo:-

· Weka lengo maalum la kusoma kila siku na litimize.
· Weka ratiba ya kila somo na ifuate.
· Uwe na mahali maalumu pa kusomea.
· Epuka kitu chochote kinachoweza kukufanya usisome vizuri.
· Usifanye mambo mengi kwa wakati mmoja. Kwa mfano, mapenzi au anasa za kimwili wakati ungali mwanafunzi. Hivyo ni vikwazo masomoni.
· Tafuta mahali pasipo na kelele za aina yoyote.
· Epuka vishawishi vinavyoweza kukufanya uahirishe kujisomea.
· Kabla hujaanza kujisomea, hakikisha kuwa zana zote muhimu kwa kusomea zipo.
· Hakikisha kuwa mahali pa kusomea pana mwanga wa kutosha.
· Unapokuwa na matatizo kimasomo, mwone mwalimu anayehusika.
· Uwe na muda mwingi wa kujisomea kila siku, usipoteze muda kwa mambo yasiyo ya lazima kama vile maongezi.
· Jiandae kwa mtihani kila wakati, usingoje mwalimu atangaze kuwa ataleta mtihani ndipo usome.
· Epusha kusoma hadi usiku sana,  utaharibu afya yako.
· Hudhuria shughuli zote za shule nje ya darasani.
· Jenga tabia ya uvumilivu na kamwe usikate tamaa wakati ugumu unapoibuka masomoni.
· Jenga tabia ya kupania kufaulu katika masomo yako.
· Amini kuwa utafaulu.
· Epuka kuwaonea wivu na kujilinganisha na wengine kimasomo, bali, jifunze tu siri za mafanikio yao.
· Chunguza masomo yao ili ujue udhaifu wako uko wapi.
· Fika darasani kwa wakati unaotakiwa ili usikose maagizo.
· Usikose kipindi bila sababu maalumu.
· Usisome mambo mengi kwa wakati mmoja.

 
· Jenga uhusiano mzuri kwa walimu wako na kwa wanafunzi wenzako. Ukiwa na amani moyoni, utasoma na kuelewa. Jistahi na kuwapenda walimu wako. Ukimpenda mwalimu utalielewa vizuri somo lake.
· Jijengee tabia njema ya kujizuia katika tamaa za mwili.
· Wasilisha kazi za darasani kwa wakati wake.
· Epuka kukaa kimya na nyuma ya darasa, bali shiriki katika mazungumzo ya darasani na wenzako.
· Uwe na muda wa kupumzika kila unapochoka kusoma.
· Epuka kusoma ukiwa umejilaza kitandani.
· Fanya mazoezi ya mwili mara kwa mara.
· Baada ya kipindi, pitia yale uliyojifunza.
· Wakati mwalimu hajafika darasani, pitia yale uliyojifunza kipindi kilichopita.
· Jisomee katika muda unaodhani unafaa zaidi.
· Tenga muda wa kutosha kwa kila somo.
· Jiwekee muda wa kutosha kila siku kwa ajili ya kazi za utoaji taarifa za masomo na projekti.
· Kama unajifunza lugha ya kigeni, fanya marudio, mazoezi mengi na soma vitabu vingi vya hadithi vya lugha hiyo.
· Soma ukiwa na kamusi na tafuta maana ya neno usilolijua.
· Jizoeze kusikiliza na kuongea ukiwaiga wajuao ujifunzapo lugha ya kigeni.
· Sikiliza mihadhara na redio ili ujifunze kwa wengine wanavyotamka maneno.
· Jikumbushe maneno magumu kila siku.
· Kila nafasi unayoipata itumie kwa kusoma.
· Pambana na sarufi za lugha ya kigeni kikamilifu.
· Jifunze lugha ya kigeni kwa kuongea mara kwa mara.
· Ni jambo la busara kuwa na usiku mmoja wa kupumzika katika juma ambayo si Jumapili au Jumamosi.
· Ni muhimu kujihusisha na watu wengine, jambo hili litakufariji kimawazo.
· Ni vizuri pia kuwa na mwanafunzi mwenzio wa kujadili naye.
· Soma kazi zako zote za darasani kabla ya kuanza darasa.
· Usiwe mtu wa kukaa tu darasani, uliza na jibu maswali yanapoulizwa.
· Uwe mwanafunzi mdadisi wa mambo kwa walimu na hata kwa wanafunzi wenzako pia.
· Epuka marafiki wabaya wenye nia ya kukupotosha.
· Epuka pombe, uvutaji wa sigara, bangi na madawa ya kulevya. Huharibu ubongo na kudhoofisha afya.
· Kabla ya mtihani, soma kwa bidii sana usingoje mtihani umekaribia ndipo usome.
· Usiku unaofuatiwa na siku ya mtihani uwe na muda wa kutosha wa kulala. Usisome hadi usiku wa manane.
· Soma kwa mpangilio kila siku ili kujiandaa kikamilifu kwa mtihani.
· Siku ya mtihani, usifikirie kushindwa bali uwe na imani kuwa utashinda. Ondoa wasiwasi na mashaka.
· Wahi kwenye chumba cha mtihani kwani kuchelewa huleta hofu.
· Chukua vifaa vyote muhimu katika mtihani kama vile kalamu, penseli na rula.
· Soma maagizo ya mtihani kwa uangalifu sana, na hakikisha uko makini kwa kile unachotakiwa kufanya kabla ya kujibu swali lolote.
· Kabla hujaanza kujibu maswali, angalia maswali ambayo ni rahisi kwako kujibu.

 
· Jibu maswali rahisi kwanza na kwa haraka ili upate muda wa kutosha kujibu maswali magumu.

Share:

1 comment:

KANUNI ZA KUSOMA NA KUFAULU

Kila mwanafunzi anahitaji kufaulu katika mitihani yake. Walimu nao hujisikia vizuri wakati wanafunzi wao wanapofanya vizuri katika miti...

ads

Hussein

Hussein + Hassan Mussa Kileo
Hussein Mussa. Powered by Blogger.
GOLDENTHINKERZ

Facebook

GOLDEN THINKERZ

Ask a question

Name

Email *

Message *

golden team

Powered By Blogger

Random Posts

Recent Posts

Popular Posts

AddsOn

AddsOn
AddsOn

Blog Archive

Recent Posts

Unordered List

Theme Support