1. IMANI YA KIISLAMU.
1.1. Dhana ya Imani katika Uislamu.
§
Maana ya
Tawhiid.
- Ni fani inayohusiana na imani ya kuwepo Allah
(s.w) na siku ya mwisho pamoja na vipengele vyote vya nguzo za imani.
- Ni kumpwekesha Allah (s.w) katika kila kitu
kwa Upweke na Umoja wake na uweza wake juu ya kila kitu.
§
Matapo
(makundi) ya Tawhiid.
- Tawhiid imegawanyika makundi makuu matatu:
1) Tawhiid – Rubbuubiyya: Ni Kumpwekesha Allah (s.w) katika Utawala
wake.
2) Tawhiid – Asmaa Wassifaat:
Kumpwekesha Allah katika Majina na Sifa zake.
3) Tawhiid
– Ibaadah: Kumpwekesha Allah (s.w) katika Uungu na Kuabudiwa.
§
Maana ya
imani kwa mujibu wa Qur’an (Uislamu).
- Ni kuwa na
yakini moyoni juu ya kuwepo kitu au jambo fulani lisiloonekana kwa macho bali
kwa dalili zinazothibitisha kuwepo kwake.
§
Imani kwa
mtazamo wa Uislamu na ule wa dini zingine:
- Katika Uislamu imani ni ile inayodhihirishwa
katika vitendo vya mtu tofauti na dini zingine.
- Katika Uislamu imani juu ya kitu au jambo
fulani lisiloonekana hutokana na dalili au ushahidi wa kuonesha uwepo wake
tofauti na dini zingine.
1.2. Nguzo za Imani.
§
Nguzo za
imani ya Kiislamu ni Sita:
1.
Kumuamini Mwenyezi Mungu (s.w).
2.
Kuamini Malaika wa Mwenyezi Mungu (s.w).
3.
Kuamini Vitabu vya Mwenyezi Mungu (s.w).
4.
Kuamini Mitume wa Mwenyezi Mungu (s.w).
5.
Kuamini Siku ya Mwisho.
6.
Kuamini Qadar ya Mwenyezi Mungu (s.w) kuwa kheri na
shari vyote vinatokana kwake.
Rejea Qur’an (2:285), (4:136), (57:22) na (11:6).
§
Nguzo ya
Ihsani.
- Nayo ni ‘kumuabudu
Allah (s.w) kana kwamba unamuona na kama
humuoni basi yeye anakuona’.
§
Nani
muumini wa kweli? (Sifa za muumini wa kweli).
- Ni yule ambaye
imani yake inathibitishwa katika matendo ya kila kipengele cha maisha yake ya
kila siku.
Rejea Qur’an
(2:8-9).
- Ni yule
anayejipamba na sifa za waumini zilizoainishwa katika Qur’an na Sunnah katika
kukiendea kila kipengele cha maisha yake ya kila siku.
Rejea Qur’an
(23:1-11), (25:63-77), (33:35-36), n.k.
- Ni yule
anayeendea kila kipengele cha maisha yake kwa mujibu wa vipengele vyote vya
nguzo za imani ya Kiislamu.
o
Hawi muumini wa kweli kwa imani isiyoendana na
matendo wala kwa kuamini baadhi ya nguzo za imani.
Zoezi la 2.
1.
(a) Nini maana
ya ‘imani’?
(b) Orodhesha nguzo za imani kwa
mpangilio wake.
(c) Ni ipi nguzo ya ‘Ihsani’?
2.
(a) Eleza maana
ya Tawhiid?
(b) Bainisha matapo au makundi ya
Tawhiid.
3.
Nani muumini wa kweli kwa mtazamo wa Kiislamu?
4. “Wenye kuamini kweli kweli ni wale waliomuamini
Mwenyezi Mungu na Mtume wake, kisha wakawa si wenye shaka, na wakapigania dini
ya Allah kwa mali
zao na nafsi zao……..” (49:15).
Kutokana na aya hii, chambua sifa kuu nne za waumini wa kweli.
5. “Na katika watu wako wasemao tumemuamini
Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho na hali ya kuwa si wenye kuamini” (2:8).
Pamoja na kudai kwako kuwa wao ni waumini (wameamini) lakini Allah (s.w)
anatufahamisha kuwa hawajaamini, kwa nini? Eleza kwa ufupi.
BY MEEK HMK CLICKER
0 comments:
Post a Comment