Kila mwanafunzi anahitaji kufaulu katika mitihani yake. Walimu nao
hujisikia vizuri wakati wanafunzi wao wanapofanya vizuri katika mitihani yao.
Sasa mtu anaweza kujiuliza, kwa nini wanafunzi wengine washindwe
na wengine wafaulu vizuri katika masomo na mitihani yao? Mafanikio katika
masomo na kufaulu mitihani kunahitaji uwezo wa asili, kufanya kazi kwa bidii na
kufuata kanunina mbmu za kusoma.
Wanafunzi wengine huona ugumu katika masomo na kufaulu mitihani,
si kwa sababu hawana akili, bali hawafuati mbinu na kanuni fulani za kusoma na
kufaulu mitihani. Wengi wana uwezo mzuri, kama watajifunza mbinu hizi. Mbinu na
kanuni hizi zinaweza kutumiwa na wanafunzi wa shule za msingi, markaz za dini,
sekondari vyuo na hata vyuo vikuu.
Kanuni za Kusoma ni kama ifuatavyo:-
· Weka lengo maalum
la kusoma kila siku na litimize.
· Weka ratiba ya
kila somo na ifuate.
· Uwe na mahali
maalumu pa kusomea.
· Epuka kitu
chochote kinachoweza kukufanya usisome vizuri.
· Usifanye mambo
mengi kwa wakati mmoja. Kwa mfano, mapenzi au anasa za kimwili wakati ungali
mwanafunzi. Hivyo ni vikwazo masomoni.
· Tafuta mahali
pasipo na kelele za aina yoyote.
· Epuka vishawishi
vinavyoweza kukufanya uahirishe kujisomea.
· Kabla hujaanza
kujisomea, hakikisha kuwa zana zote muhimu kwa kusomea zipo.
· Hakikisha kuwa
mahali pa kusomea pana mwanga wa kutosha.
· Unapokuwa na
matatizo kimasomo, mwone mwalimu anayehusika.
· Uwe na muda mwingi
wa kujisomea kila siku, usipoteze muda kwa mambo yasiyo ya lazima kama vile
maongezi.
· Jiandae kwa
mtihani kila wakati, usingoje mwalimu atangaze kuwa ataleta mtihani ndipo
usome.
· Epusha kusoma hadi
usiku sana, utaharibu afya yako.
· Hudhuria shughuli
zote za shule nje ya darasani.
· Jenga tabia ya
uvumilivu na kamwe usikate tamaa wakati ugumu unapoibuka masomoni.
· Jenga tabia ya
kupania kufaulu katika masomo yako.
· Amini kuwa
utafaulu.
· Epuka kuwaonea
wivu na kujilinganisha na wengine kimasomo, bali, jifunze tu siri za mafanikio
yao.
· Chunguza masomo
yao ili ujue udhaifu wako uko wapi.
· Fika darasani kwa
wakati unaotakiwa ili usikose maagizo.
· Usikose kipindi
bila sababu maalumu.
· Usisome mambo
mengi kwa wakati mmoja.
· Jijengee tabia
njema ya kujizuia katika tamaa za mwili.
· Wasilisha kazi za
darasani kwa wakati wake.
· Epuka kukaa kimya
na nyuma ya darasa, bali shiriki katika mazungumzo ya darasani na wenzako.
· Uwe na muda wa
kupumzika kila unapochoka kusoma.
· Epuka kusoma ukiwa
umejilaza kitandani.
· Fanya mazoezi ya
mwili mara kwa mara.
· Baada ya kipindi,
pitia yale uliyojifunza.
· Wakati mwalimu
hajafika darasani, pitia yale uliyojifunza kipindi kilichopita.
· Jisomee katika
muda unaodhani unafaa zaidi.
· Tenga muda wa
kutosha kwa kila somo.
· Jiwekee muda wa
kutosha kila siku kwa ajili ya kazi za utoaji taarifa za masomo na projekti.
· Kama unajifunza
lugha ya kigeni, fanya marudio, mazoezi mengi na soma vitabu vingi vya hadithi
vya lugha hiyo.
· Soma ukiwa na
kamusi na tafuta maana ya neno usilolijua.
· Jizoeze kusikiliza
na kuongea ukiwaiga wajuao ujifunzapo lugha ya kigeni.
· Sikiliza mihadhara
na redio ili ujifunze kwa wengine wanavyotamka maneno.
· Jikumbushe maneno
magumu kila siku.
· Kila nafasi
unayoipata itumie kwa kusoma.
· Pambana na sarufi
za lugha ya kigeni kikamilifu.
· Jifunze lugha ya
kigeni kwa kuongea mara kwa mara.
· Ni jambo la busara
kuwa na usiku mmoja wa kupumzika katika juma ambayo si Jumapili au Jumamosi.
· Ni muhimu
kujihusisha na watu wengine, jambo hili litakufariji kimawazo.
· Ni vizuri pia kuwa
na mwanafunzi mwenzio wa kujadili naye.
· Soma kazi zako
zote za darasani kabla ya kuanza darasa.
· Usiwe mtu wa kukaa
tu darasani, uliza na jibu maswali yanapoulizwa.
· Uwe mwanafunzi
mdadisi wa mambo kwa walimu na hata kwa wanafunzi wenzako pia.
· Epuka marafiki
wabaya wenye nia ya kukupotosha.
· Epuka pombe,
uvutaji wa sigara, bangi na madawa ya kulevya. Huharibu ubongo na kudhoofisha
afya.
· Kabla ya mtihani,
soma kwa bidii sana usingoje mtihani umekaribia ndipo usome.
· Usiku unaofuatiwa
na siku ya mtihani uwe na muda wa kutosha wa kulala. Usisome hadi usiku wa
manane.
· Soma kwa mpangilio
kila siku ili kujiandaa kikamilifu kwa mtihani.
· Siku ya mtihani,
usifikirie kushindwa bali uwe na imani kuwa utashinda. Ondoa wasiwasi na
mashaka.
· Wahi kwenye chumba
cha mtihani kwani kuchelewa huleta hofu.
· Chukua vifaa vyote
muhimu katika mtihani kama vile kalamu, penseli na rula.
· Soma maagizo ya
mtihani kwa uangalifu sana, na hakikisha uko makini kwa kile unachotakiwa
kufanya kabla ya kujibu swali lolote.
· Kabla hujaanza
kujibu maswali, angalia maswali ambayo ni rahisi kwako kujibu.